Sunday, March 25, 2012

SIMBA SC YAIRARUA ES SETIF 2-0

 Mashabiki wa Simba kabla ya mchezo.

Kikosi cha Simba kilichowaua Waarabu leo.

Felix Sunzu kazini.

 Salum Machaku (katikati) akisikilizia maumivu.

 Waheshimiwa Fredric Sumaye, Said El-Maamry, Zitto Kabwe na Aden Rage wakiipa sapoti Simba SC.
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC leo wameirarua ES Setif kutoka nchini Algeria kwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, uliopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba yamefungwa na Emmanuel Okwi pamoja na Haruna Moshi.

Basi la Super Najmunisa lateketea kwa moto jioni ya leo Mkoani Morogoro

 Basi la Abiria la kampuni ya Super Najmunisa lifanyalo safari zake kati ya Dar es Salaam na Mwanza. likimalizikia kuteketea kwa moto mara baada ya kupata shoti ya betri.ajali hiyo imetokea jioni ya leo maeneo ya Berege Mkoani Morogoro wakati basi hilo likiwa njiani kuelekea jijini Dar es Salaam kutokea Mwanza. hakuna mtu yeyote aliedhulika kwenye ajali hiyo isipokuwa mizigo yote ya abiria hao iliteketea kwa moto.

 Basi hilo nikiendelea kuwaka moto.

 Sehemu ya Abiria wa Basi hilo pamoja na wamazi wa maeneo ya jirani na kijiji hicho wakiwa wamekaa pembeni kuangalia jinsi gari hilo linavyoteketea kwa moto bila ya wao kujua la kufanya wakati huo.

FAMILIA YA KAJALA YAKATAA MCHANGO WA WEMA

 KUFUATIA kesi ya kughushi hati ya fedha inayomkabili mumewe, Faraji Augustine Chambo, staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja, 26, aliyeko Gereza la Segerea, Dar es Salaam akisubiri hukumu, baadhi ya ndugu zake wameibuka na kudai kuwa hawahitaji kuona mchango wa mwigizaji mwenzake, Wema Sepetu.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha Risasi Jumamosi, tamko hilo limekuja baada ya baadhi ya wasanii kuanza kuchangishana fedha kwa ajili ya kumuwekea dhamana Kajala ili asiendelee kusota gerezani.

 

NI UNAFIKI?

“Wema ndiye alikuwa mara nyingi akifurahia ndugu yetu kuhukumiwa, hivi karibuni alikuwa akimsema vibaya hadi kufikia hatua ya kugombana naye, atuletee mchango? Utakuwa ni unafiki tu hata hatuhitaji,” alisema ndugu wa karibu wa familia ya Kajala.
HUKUMU
Hukumu ya kesi hiyo iliahirishwa juzi Alhamisi hadi Jumatatu ijayo Machi 26, mwaka huu.
TUJIKUMBUSHE
Leo Kajala ametimiza siku nane tangu alipotupwa katika Gereza la Segerea Machi 16, mwaka huu ambapo alishikiliwa na maofisa wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa madai kuwa aliuza nyumba ya mumewe Faraji iliyokuwa na mgogoro ambayo walikuwa wakiichunguza maeneo ya Mbezi Salasala, Dar.

 WEMA ANASEMAJE?
Risasi Jumamosi lilimsaka Wema kwa njia ya kilongalonga cha kiganjani ili kumfikishia habari hiyo na kusikia anasemaje, lakini juhudi hizo ziligonga mwamba kufuatia simu yake kutokuwa hewani kila ilipopigwa.

UWOYA adhalilika

 IKIWA ni siku chache tangu mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ alipoondoka Bongo, Irene Pancras Uwoya anadaiwa kudhalilika ukumbini baada ya kigauni kifupi alichotinga kushindwa kumsitiri hivyo ‘kufuli’ lake kuwa nje nje, aya zifuatazo zina undani kamili.

Tukio hilo la kusikitisha lilichukua nafasi ndani ya Ukumbi wa Business Park Kijitonyama, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo kulikuwa na ‘bethidei’ ya mwaka mmoja ya Klabu ya Bongo Movie.

MAPEDESHEE WAJIPITISHA
‘Shushushu’ wa gazeti hili aliwashuhudia wanaume hasa mapedeshee wakijipitisha mbele ya meza aliyokuwa amekaa Uwoya na mwigizaji mwenzake, Blandina Chagula ‘Johari’.
Hata hivyo, ilielezwa kuwa kilichomponza Uwoya ni kigauni alichovaa kifupi kilichosababisha nguo hiyo ya ndani nyeupe kuonekana kirahisi alipokuwa amekaa.
NENO LA WADAU
“Duh! Mama Krish (Uwoya) katoka bomba lakini kile kigauni kinamdhalilisha, kinaonesha kufuli yake nyeupe.
Ukweli ni kwamba angekuwepo Ndiku (mumewe) asingefanya hivyo kwa sababu angemlindia heshima,” alisema mmoja wa wadau waliomshuhudia staa huyo ambaye muda mwingi alikuwa kimya ukumbini humo.
UWOYA VIPI?
Jitihada za kuzungumza na Uwoya juu ya tukio hilo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kuita bila kupokelewa.
Hivi karibuni Ndiku alitimka Bongo na kwenda kwao Rwanda kujiunga na timu ya Rayon Sports huku akimwacha mkewe huyo na mwanaye Krish. 

Mtu na wifi yake wanaswa wakijiuza

UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni, sakata la mtu na wifi yake kunaswa wakifanya biashara ya ukahaba na kufikishwa mahakamani limewastajabisha wengi, Risasi Jumamosi linakutaka ukae mkao wa kula kupata kisa hiki.

 Sakata zima liko hivi, Jennipher Anthony (21) Mkazi wa Tabata jijini Dar pamoja na wifi yake Mgeni Tumaini (35) Machi 13, mwaka huu saa 9 usiku  walinaswa  na polisi maeneo ya Buguruni  Kwasokota jijini Dar wakiwa katika harakati za biashara yao ya ukahaba.

Mara baada ya kukamatwa na polisi, mtu na wifi mtu hao walipandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Sokoine Drive kwa kosa hilo.
Wakizungumza na Risasi Jumamosi, ndugu wa watuhimiwa hao waliofika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo, walimlaumu Mgeni kwa kumpotosha wifi yake Jennipher na kumuingiza kwenye biashara hiyo haramu wakati akijua kuwa ana umri mdogo.
“Jennipher ametoka Iringa kwa ajili ya kuja kutafuta maisha na kufikia kwa wifi yake, kumbe walikuwa wakifanya biashara hiyo haramu bila sisi kujua,” walisema ndugu hao kwa masikitiko.  
Mbali na Jennipher na wifi yake, wanawake wengine waliopandishwa kizimbani katika mahakama hiyo  kwa kutokana na kise hiyo ni Asha Samson (25) Mkazi wa Mburahati, Aisha Mohammed (35) Mkazi wa Kigogo pamoja na Jenny Michael (19) Mkazi wa Mbagala na kusomewa shitaka la kufanya biashara haramu ya ukahaba.
Akiwasomea mashitaka yao Kaimu Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama hiyo Richard Magodi mbele ya Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Timothy Lyon alisema washitakiwa wote kwa pamoja walikana shitaka hilo.
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo aliihairisha kesi mpaka Machi 26 mwaka huu, huku watuhumiwa wakikosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti na kupandishwa karandika kwenda katika Gereza la Segerea mpaka kesi hiyo itakapotajwa tena.

Rais Kikwete awaapisha Makatikbu Tawala wa Mikoa ikulu jijini Dar Es Salaam

 Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Mbeya Bibi.Mariam Mtunguja akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es salaam leo.Katika hafla hiyo Rais aliwaapisha pia makatibu Tawala wa mikoa mingine kama ifuatavyo,Dkt. Faisal Issa (Kilimanjaro),Bwana Eliya Ntandu (Morogoro), Bwana Severine Kahitwa (Geita),Bwana Emmanuel Kalobelo (Katavi), Bwana Hassan Bendeyeko (Ruvuma) na Dkt. Anselem Tarimo (Shinyanga).(Picha na Freddy Maro).

Davina: Wapenzi wangu wengi walikuwa wa maneno

 KARIBU tena mpenzi msomaji wa SIDE B. Leo tunamalizia kuperuzi maisha ya upande wa pili ya mwigizaji wa sinema za Bongo, Halima Yahya ‘Davina’. Ili kujua nini amemalizia fuatana nami.

VIPI KUHUSU MAUMIVU KATIKA MAPENZI?
Davina: Mwanaume akitambua unampenda sana lazima ipo siku atakuumiza tu. Kwa kweli nimeshaumizwa sana, ila kwa sasa nafasi hiyo haipo tena.
JE, ANAMKUMBUKA MPENZI WAKE WA KWANZA?
Davina: Kama nilivyokwambia mara ya kwanza kuwa nilianza kutoa uroda mara baada ya kumaliza kidato cha nne, ila wale ambao nilikuwa na mapenzi ya stori wapo wengi.
ETI ANA BIFU NA NISHA?
Davina: Hapana mimi sina bifu na Nisha, labda yeye kama anatangaza ana bifu na mimi, lakini sina muda huo.
SIDE B: Kuna tetesi zisizo rasmi kuwa Nisha ana uhusiano wa kimapenzi na mzazi mwenzako aliyesababisha ukalale mahabusu Segerea, hujasikia hilo?
DAVINA: Haitakuja kutokea kwa sababu yule mwanaume mimi ndiye niliyemuacha. We unaona shepu ya kuachwa hii, hebu nitazame vizuri kwanza, sina shida ya kumpa mtu promo kupitia jina langu.
MAJUNGU JE?
Davina: Hakuna kitu kinachoniuma kama majungu, hasa kwa sisi wanawake wa Bongo Movie. Kwa kweli tuna ushoga wa ‘Kichina’, ukiwa naye anakuwa rafiki, mkiachana tu anakwenda kukuweka hadharani baadaye ukija kusikia huamini masikio yako.
ANASEMAJE KUHUSU MASTAA WA KIKE KUTOA URODA ILI WAPEWE NAFASI YA KUIGIZA?
Davina: Siwezi kuongopa, ni kweli hilo suala lipo na mimi nilishawahi kukumbana nalo, si kwenye sanaa tu hata maofisini mambo hayo yapo, mashuleni pia hayaepukiki.
MSOSI UNAOUZIMIA
Davina: Sina chaguo kwenye kula, napenda vyakula vingi.
ANAPENDA MWANAUME WA AINA GANI?
Davina: Napenda mwanaume mwenye mvuto, anayejua kumuenzi mpenzi wake na awe mtundu ‘uwanjani’ kipindi cha mechi.
NJE YA UIGIZAJI ANAFANYA NINI?
Davina: Kwa sasa sina ninalolifanya nje ya kuigiza lakini nina mpango wa kumiliki kampuni yangu pamoja na taasisi ambayo itawasaidia kina mama kujikwamua kimaendeleo.
KITU GANI ANACHOKIKUMBUKA KILA WAKATI?
 Davina: Ni siku niliyopanda karandinga kwenda Segerea, najuta maana mapenzi ndiyo yaliyonifanya nikalale kule, nisingekuwa na uhusiano na yule mtu hadi kuzaa naye nisingepata matatizo yale.
“Asikwambie mtu jela isikie tu kwa mwenzako, lakini usiombe ikukute wewe, ni kubaya mno hakufai hata kuhadithiwa.”
SIDE B: Nashukuru sana kwa ushirikiano wako Davina, Mungu akupe afya njema.
Davina:  Ahsante.

Unapoamua kupenda, vaa uvumilivu, ikibidi kubali kuwa bwege

 Mada hii ina lengo la kukufanya uyaelewe mapenzi. Si kukimbilia kuacha pale kunapotokea tofauti za hapa na pale na mwenzi wako wa maisha. Uvumilivu unahitajika, amini kwamba utamu wote unaoyazunguka ‘malavidavi’ kuna ugumu mkubwa.

Ni sehemu ya tatu. Hapa tunazungumzia elimu zaidi inayoweza kukukomboa wewe kwa kuheshimu hisia za mwenzako na wakati huohuo ukawa unajali za kwako. Kwa pamoja ndipo utaweza kufanikiwa kuwa na moyo tulivu katika nyakati zote.
Ukiheshimu hisia za mwenzi wako na ukawa unajali za kwako, itakusaidia kukufanya uwe na tumaini chanya wakati wote. Wakati wa matatizo, hasa kipindi ambacho hampo kwenye maelewano mazuri, utabaki na imani kwamba yote yatakwisha.
Penda kuamini kuwa “hili nalo litapita” kwamba wakati ambao mwenzi wako amenuna, hataki kuzungumza na wewe, unachopaswa kufanya ni kuheshimu hisia zake na uamini kwamba mwisho atatulia na uhusiano wenu utaendelea kwa maelewano makubwa.
Ukitaka kulazimisha awe mchangamfu kwako kipindi ambacho amenuna, ni sawa na kukaribisha matatizo zaidi. Ni vema kuelewana, watu wengi wanakosea katika uhusiano wao kwa sababu hawatumii busara ili kuwaelewa wenzi wao pindi wanapoonesha hali tofauti.
Busara iendelee kuchukua nafasi. Maneno “hili nalo litapita” yawe somo kwako. Kwamba leo umerudi nyumbani, umetaka chakula cha faragha, mwenzako amekwambia hajisikii vizuri. Hutakiwi kupandisha mizuka na kusababisha nyumbani pasilalike kwa siku hiyo.
Badala yake unapaswa kuvumilia. Jiulize mmefanya tendo mara ngapi katika uhusiano wenu, iweje siku hiyo akwambie hajisikii? Ukilazimisha ni sawa na kumfanyia mwenzako ubakaji. Si ajabu akiona unakuwa mkali, akakubali kukupa kwa shingo upande lakini si kwa ridhaa yake.
Mapenzi ni matamu lakini siyo rahisi kwa maana nyakati nyingine utalazimika kuvumilia mambo ambayo pengine yakakuumiza. Mpo wawili na kujenga tafsiri ya mwili mmoja. Pengine hata makundi yenu ya damu ni tofauti. Ilivyo maumbile yenu ni hasi na chanya ndiyo na damu zenu zilivyo.
Tofauti hiyo mnaielewa na kuikubali, iweje siku ukirudi nyumbani unamkuta amenuna na hataki kuzungumza na wewe ushindwe kuelewa? Hapo ndipo uvumilivu wako unahitajika. Ni kipindi ambacho busara zako zinapaswa kufanya kazi kwa asilimia 100. Usilazimishe afanye upendavyo wakati mwili wake haupo tayari.
Unaingia faragha na mwenzi wako. Ameshindwa kukuridhisha kabisa. Ni hekima zako kutambua kwamba siku hazilingani. Mbona siku nyingine alikupa mambo mazuri mpaka ukasema ‘poo’? Tatizo ni nini? Pengine nishati za mwili wake kwa siku hiyo hazipo sawasawa na hata yeye mwenyewe hajui.
Ukimkejeli kuwa hajiwezi ni sawa na kumchinjia baharini. Siku zinazokuja atashindwa kabisa. Si kwa sababu uwezo wake ni mdogo, la hasha! Maneno yako ya kejeli na dharau ndivyo vitakavyoufanya moyo wake usinyae na kukuogopa ndani kwa ndani. Fikra zake zitashambuliwa na ugonjwa hatari.
Si ugonjwa unaosababishwa na kirusi, hapana. Ni gonjwa la maneno litakaloshambulia ubongo wake. Kila mara kabla ya kuingia mchezo atakuwa na maswali ya kujiuliza: “Sijui leo nitashindwa tena?” “Nikishindwa itakuwaje?” “Atanitukana tena?”  “Hivi mimi ni mgonjwa?”
Mwisho wa maswali hayo atahitimisha kauli kwa kusema: “Inawezekana mimi ni mgonjwa kweli ndiyo maana nashindwa kazi.”

Mchungaji anaswa akimuogesha mke wa mtu

AMA KWELI dunia imekwisha, makanisa, watumishi wa Bwana wanazidi kumtia hasira Mungu kila kukicha, Afrika ndiyo inaongoza. Mtumishi mmoja wa Mungu nchini Ghana amenaswa hivi karibuni akimwogesha mke wa mtu ambaye ni muumini wake kwa madai anamtakasa.
Picha ya mtumishi huyo ilipigwa kwa siri na kamera ndogo iliyotegwa eneo la tukio.
Habari zinasema mtumishi huyo (jina lake halikupatikana mara moja) alimwogesha mwanamke huyo wakati wa mfululizo wa maombi ya utakaso maarufu kwa jina la Deliverensi.
Baada ya kumaliza kumwogesha, alimfuta maji kwa taulo na baadaye kumpaka mafuta aliyodai yana upako wa ki-Mungu ‘Anointed’.
Ni vyema jamii ikaangalia upya sera za makanisa, hasa ya kiroho, wanayojiunga nayo kwani mengi hayafuati maagizo ya Mungu bali shetani.
NI AIBU SANA

STORI; MAKONGORO OGING NA ISSA MNALY
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni! Mwanamke mmoja jijini Dar es Salaam aliyetajwa kwa jina moja la Kesi ameibua timbwili zito baada ya kutwangana na bintiye Eliza wakidaiwa kugombea mwanaume, Ijumaa linakupa kisa na mkasa.
 NI TANDALE
Tukio hilo ambalo ni aibu isiyopimika lilifunga mtaa nyumbani kwa mama huyo maeneo ya Tandale Mbuyuni, Dar hivi karibuni baada ya Eliza kumtuhumu mama yake mkubwa kuwa anatembea na bwanaa’ke.
Wakiwa kwenye pilikapilika za kazi zao, waandishi wetu walipigiwa simu na chanzo ambacho kilidondosha habari juu ya sekeseke ambalo lilikuwa linanukia kutokea maeneo hayo la mama na mtoto kutwangana kisa mwanaume.
Ijumaa lilipotimba kwenye eneo la tukio, lilikuta umati ukiwa umejazana huku magari, Bajaj, pikipiki na baiskeli zikiwa hazina pa’ kupita.
 PAMBANO LAIVU, WATU WASEREBUKA
Wakati wawili hao wakitwangana laivu, baadhi ya majirani, hasa akina mama walikuwa wakishangilia kwa kupiga ndoo kama ngoma huku wakiserebuka kwa furaha.
Ilibidi kuhoji majirani kulikoni watu kutwangana na wengine kufurahia ambapo walidai kuwa wamechoshwa na visa vya mama na mwanaye kuchukuliana mabwana.
 MAMA ACHOROPOKA
Hata hivyo, mama huyo alifanikiwa kuchoropoka mikononi mwa bintiye baada ya kuzidiwa na kipigo ambapo alitoka nduki huku watu wakimkimbiza kwa kushangilia.
 BINTI HEWANI LAIVU
Akizungumza na Ijumaa baada ya ‘mbaya’ wake kumchomoka huku akibubujikwa na machozi, binti huyo alisema kuwa siku moja kabla ya sekeseke hilo namba ya simu ya mama yake ilimpigia saa 4:30 usiku.
“Cha kushangaza, nilipopokea sauti ya upande wa pili haikuwa ya mama bali ilikuwa ya mwanaume wangu,” alisema binti huyo kwa uchungu.
 Alisema kuwa jamaa huyo alikuwa akiongea kwa kujiamini na nyodo akimuuliza mpigaji ni nani na kwa nini alipiga simu usiku huo kwani wao wamelala, hawataki usumbufu.
“Niliielewa vizuri sauti ya bwanaa’ngu kwani tumeishi pamoja muda mrefu na tuna mtoto wa mwaka mmoja na nusu, nilishangaa sana, nilipomuuliza mama unalala na bwanaa’ngu, bila shaka akashtuka na kunijibu kwa kubabaika, “ alisema.
 Alisema kuwa siku ya tukio hilo, wakati akiwa nyumbani hapo akimsubiri mama yake huyo ambaye alilala kwa bwanaa’ke huyo, alipigiwa simu na  mwanaume huyo na kumweleza kuwa hivi sasa yupo na mama hivyo yeye akae pembeni.
Baada ya kutia timu nyumbani, ndipo pakachimbika na kuzuka kwa timbwili hilo.
Hadi gazeti hili linang’oa nanga eneo la tukio mama huyo alikuwa hajarejea nyumbani baada ya kupokea kichapo ‘hevi’.
DK Slaa amshangaa mkapa
Waandishi Wetu, Arumeru
 KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amemshambulia Rais mstaafu, Benjamin Mkapa na wabunge wa CCM kwa kile alichodai kuwa ni kuendesha kampeni zilizojaa uongo katika jimbo la Arumeru Mashariki na kwamba viongozi hao wanashusha hadhi ya Serikali.

Chadema kilifanya mkutano wake wa mwisho jana kwenye uwanja wa michezo wa Ngaresero ambako CCM walizindulia kampeni zao zilizoongozwa na Mkapa, Machi 12, mwaka huu.

Dk Slaa alisema kama viongozi wakubwa wa kitaifa wakiwa ni watu wa kusema uongo haiwezekani nchi kupata maendeleo.

“Alikuja kwenye uwanja huu, Rais mstaafu Mkapa, badala ya kusema mgombea wao akichaguliwa atafanya nini anaanza kusema Vincent Nyerere hatoki katika ukoo wa Nyerere ,….baada ya kumkosoa anaomba radhi lakini wenzake wanasambaza waraka eti Vincenti hakuzaliwa katika familia ya Nyerere,” alisema Dk Slaa.

Alisema wana CCM hao, wametoa tuhuma za kipuuzi eti, Vincent ambaye ni mtoto wa mwisho kuwa mama yake alikwenda naye kwa marehemu baba yake, Josephat Kiboko Nyerere .

“Ndugu zangu jiulizeni Vincent ni mtoto wa mwisho sasa hata kwa akili ya mtoto kweli unaweza kuhamia kwa mwanaume ukiwa tayari umezaa watoto wanne,” alihoji Dk Slaa.

Dk Slaa alisema kwa upande wa Wassira, amekuwa akimtuhumu kuwa ameiba fedha za ujio wa Papa mwaka 1991 kitu ambacho ni uongo wa mchana na licha ya kuelezwa ukweli na viongozi wa Kanisa Katoliki, ameng’ang’ania kuwa ameiba.

“Sasa mimi nahoji kama kweli nimeiba tangu mwaka 1991 na Serikali ya CCM imeshindwa kunikamata basi ikiri kuwa Serikali yake ni dhaifu, “alisema Dk Slaa.

Dk Slaa pia alimshambulia Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani kwa kutoa taarifa za uongo juu ya kufika kambi ya Chadema na kukumbatiana na mgombea Joshua Nassari na baadaye akakana na kudai gazeti hili limetengeneza picha yake huku akidai mgombea wa chadema ametishia kumuua na kumchoma moto.

“Leo(jana) Mwananchi wametoa picha tofauti ambazo zinaonyesha akiwa katika kambi ya Chadema na akikumbatiana na wanachama wa Chadema na huu ndio uongo wa viongozi hawa wa CCM,” alisema Dk Slaa.

Aliwaomba wapiga kura wa jimbo hilo kumchagua Nassari ili akadhibiti ufujaji wa fedha katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru akimfananisha na paka mwenye uwezo wa kudhibiti panya wengi wanaokula mazao ghalani.

Katika hatua nyingine, Dk Slaa alisema chama chake kimegundua makosa ya baadhi ya majina ya wapiga kura kufutwa kwenye orodha ya wapiga kura na kuwataka wananchi kwenda kwenye vituo vya kupigia kura kuhakiki majina yao na kutoa taarifa kwa viongozi wa Chadema kwenye maeneo yao ili hatua za haraka zichukuliwe kurekebisha makosa hayo ambapo kwa jimbo zima, alisema majina 55 yameondolewa bila maelezo.

Amvaa Lowassa
Katika mikutano ya jana, Dk Slaa alimvaa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kwa kumtaka kujitokeza hadharani kwenye majukwaa ya siasa, badala ya kufanya kampeni za mafichoni.

Akimnadi mgombea wa chama hicho, Nasaari eneo la Malula, Kata ya Kikatiti jana, Dk Slaa alidai kuwapo kwa taarifa kwamba Lowassa amekuwa akipita kimya kimya mitaani kumpigia kampeni mkwewe, Sioi huku akitumia chakula cha msaada kama rungu la kuwatishia wapiga kura.

“Kama Lowasa ni mwanaume kweli ajitokeze hadharani, apande jukwaani kushiriki siasa Arumeru ili Chadema tumtendee haki kwa kumpatia vidonge vyake kwa sababu yeye alishawakana Wameru kwa kukana kabila lake la Meru na kujifanya Mmaasai, leo anakuja hapa kuwadanganya na kuwatisha kwa ajili ya maslahi ya mkwe wake Sioi ili kuongeza idadi ya mafisadi bungeni,” alisema Dk Slaa.

Dk Slaa alisema Lowassa akiwa mbunge wa Monduli (CCM) anapaswa kwanza kuchukua hatua za kudhibiti wizi na ubadhirifu unaofanywa ndani ya Halmashauri ya Monduli ambao ulibainishwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), huku kamati hiyo ikitaka wahusika wafikishwe mahakamani.

Kauli ya Dk Slaa kuhusu Lowassa imekuja wakati kukiwa na taarifa kwamba mbunge huyo wa Monduli huenda akapanda jukwaani leo kumnadi Sioi.

Mratibu wa kampeni za CCM, katika jimbo la Arumeru Mashariki, Mwigulu Nchemba alisema jana kuwa Lowassa anatarajia kupanda jukwaani wakati wowote na kwamba kwa siku atakuwa akifanya mikutano kati ya miwili na mitatu kumnadi Sioi.

Hata hivyo Mwigulu hakuwa tayari kutaja siku ambayo Lowassa ataanza kampeni hizo, lakini watu walio karibu na kiongozi huyo walisema huenda akaanza kusimama jukwaani leo.

Mwiguli alisema CCM kilikuwa kinafanya mawasiliano na mbunge huyo kwa lengo la kumjumuisha kwenye ratiba ya kampeni na kwamba ujio wake utaiongezea nguvu timu hiyo.

Wakati hayo yakiendelea, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe naye anatarajiwa kupanda rasmi jukwaani leo kuongeza nguvu kwenye kampeni za chama chake.

Mbowe anajiunga na timu ya kampeni baada ya kuhitimisha kuongoza harambee ya kukichangia chama hicho iliyofanyika juzi usiku mjini Arusha ambako zaidi ya Sh150 milioni zilipatikana.


Imeandaliwa na Neville Meena, Mussa Juma, Peter Saramba na Moses Mashalla.
CCM yadai Matumizi helikopta Chadema ni ufisadi’
 Waandishi Wetu
WAKATI Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kikiendelea kutumia helikopta katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki, hatua hiyo imeelezwa kuwa ni ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za wanachama wake.Jana chama hicho kilifanya mikutano mitano katika kata za Leguruki, Makiba, King’ori, Maloloni na Usa River.


Akimnadi mgombea wa CCM, Sioi Sumari kwenye mikutano iliyofanyika katika vijiji vya Akheri na Patandi, mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde alisema kwa kutumia helikopta, Chadema wanafanya ufisadi kwani wamekuwa wakiwakamua wananchi fedha za uendeshaji wa chama hicho.

Lusinde alibeza matumizi ya helikopta na kusema kwamba ni kufuru kwa vile kila inapokuwa angani, inatumia Sh60 milioni.

Alisema ya kwamba helikopta hiyo kila irukapo angani kwa saa, imekuwa ikitumia kiasi cha Sh2 milioni kitendo ambacho kimekuwa kikitumia fedha zinazochangwa na wafuasi wa Chadema.

Lusinde, alisema kwamba baadhi ya wafuasi wa Chadema wamekuwa wakikamuliwa kwenye mikutano ya hadhara kuchangia gharama za usafiri wa helikopta hiyo wakati hali yao ni ngumu kimaisha.

“Ndugu wananchi ngoja niwapeni siri hawa wenzetu hawana huruma na nyie kabisa, wanawachangisha fedha za helikopta wakati kila ikiruka hewani sh,60 milioni zinawatoka kuweni makini” alisema Lusinde

Kauli ya Lusinde imekuja wakati kukiwa na taarifa za uhakika kwamba CCM kinatafuta uwezekano wa kuwa na helikopta ambayo wataitumia walau kwa siku tatu au nne za mwisho.

Mmoja wa viongozi wa chama hicho aliyepo kwenye timu ya kampeni aliliambia gazeti hili kuwa: “Helkopta pia ni siasa, si kwa ajili ya kufanya mikutano mingi tu, kwa hiyo na sisi wakubwa wetu wanahangaika ili walau siku tatu au nne za mwisho tuweze kuitumia”.

Katika uchaguzi mdogo wa Igunga uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana, vyama vya CCM, Chadema na CUF vilitumia helikopta katika kampeni za kuwanadi wagombea wao.

Gazeti lagawisha bure
Katika hatua nyingine, mamia ya nakala za gazeti la kila wiki (jina tunalihifadhi kwa sasa) jana zilikuwa zikigawiwa kwa watu waliofika kwenye mikutano ya kampeni za mgombea wa CCM, Sioi.

Gazeti hilo toleo nambari 177 la Machi 21 – 27, 2012 lina taarifa nyingi zinazohusu uchaguzi wa Arumeru na baadhi yake zinasema; Chadema wakata tamaa, ‘meseji’ za Nassari zanaswa akikiri kushindwa, Chadema waburuzana kortini wakati tahariri yake inasema Chadema waache uhuni Arumeru.

Gazeti hilo liligawanywa bure na maofisa wa CCM kwa wananchi waliofika kwenye mikutano ya King’ori, Patandi – Maji ya Chai na Leguruki na haikuweza kufahamika mara moja sababu za kufanya hivyo.

Mhariri wa gazeti hilo (pia jina tunalihifadhi) alipoulizwa alisema: "Sifahamu chochote kuhusu suala hilo, labda CCM wamenunua nakala nyingi kwa ajili ya kuwagawia watu wao lakini ngoja nifuatilie maana sikuwapo ofisini kwa wiki nzima".Mratibu wa Mkuu wa Operesheni wa Kampeni wa Chadema jimboni Arumeru Mashariki, John Mrema alisema ni dhahiri kwamba gazeti hilo linasambazwa kukichafua chama hicho na kwamba bado wanatafakari hatua za kuchukua.

Imeandaliwa na Neville Meena, Mussa Juma, Peter Saramba na Moses Mashalla.
Nyumba ya Mungu si shwari 
 Hawra Shamte
AGIZO alilolitoa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Khalid Mandya Februari 13 mwaka huu la  kufunga kwa muda shughuli za uvuvi katika Bwawa la Nyumba ya Mungu, kwa wakazi wa eneo hilo liligeuka msumari wa moto uliochoma mioyo yao.

Tamko hilo ambalo alilito wakati akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Magadini Wilaya ya Simajiro, lilikuwa ni sawa na kuwahukumu kifo, kwa sababu bwawa hilo ndilo tegemeo kubwa la maisha yao.

Wakazi wa Magadini, kijiji kinachojumuisha vitongoji vya Magadini, Majengo na Korongo si wakulima kwa sababu ardhi yao ni kame.  

Bwawa la Nyumba ya Mungu ndiyo tegemeo lao, kwa kuwa shughuli yao kuu ni uvuvi.  Hawa samaki ndio wanaowapatia unga, mafuta ya taa na mahitaji mengineyo.

“Kama hakuna samaki hata hao ng’ombe na mbuzi tunaochunga hawatusaidii, kwa sababu ni rahisi kupata fedha kutokana na samaki kuliko ng’ombe au mbuzi, hasa kwa sababu siku hizi mifugo ina matatizo mengi, magonjwa yamekuwa mengi na malisho pia yamekuwa haba,” anasema Mzee Raymond Kishia, mkazi wa Korongo.

Maji katika Bwawa la Nyumba ya Mungu yamepungua na sasa hivi samaki wanapatikana kwa shida, wapo kidogo sana na hawana ukubwa waliokuwa nao awali.

Hayo yanasababishwa na mambo mengi, mojawapo ni mabadiliko ya tabia nchi, joto limeongezeka na kuathiri viumbe hai.  Lakini pia kazi ya mikono ya binadamu;  wavuvi kwa tamaa ya kupata samaki wengi wamekuwa wakivua kwa kutumia nyavu ndogondogo (kokoro)na pia kwa kutumia vyandarua, hivyo huvua hata samaki wadogo na mazalia yao.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Korongo, Daniel Tengelemingi anasema ingawa Serikali imepiga marufuku uvuvi wa kokoro na uvuvi wa mitengo (kutumia vyandarua vyenye ngao), uvuvi huo umekuwa ukiendelea kwa kificho hasa nyakati za usiku.

“Hivi vyandarua vyenye ngao vina sumu, tena imeandikwa kabisa kuwa dawa yake haimaliziki mpaka baada ya miaka mitano au zaidi, lakini hapa wapo baadhi ya wavuvi wanaotumia vyandarua hivi na kutuingizia sumu kwenye bwawa letu,” anasema Tengelemingi.

Je, serikali ya kijiji haifahamu hali hiyo?

“Sisi tuna wasiwasi na Ofisa Uvuvi wetu, kwani wapo watu wanaoendelea na uvuvi nyakati za usiku na taarifa hizi huyu Bwana Samaki wetu anazo, lakini ametulia tuli kama hakuna kinachoendelea,” Tengelemingi anasema.

Aidha tatizo jingine linalodaiwa kuwapo kijijini hapo ni ubabe wa viongozi wake. Viongozi hao  wanadaiwa kuendesha kijiji kidikteta, neno lao ni amri wamejigeuza kuwa ni mahakama na pia wanawaweka ndani watuhumiwa kwa muda wanaotaka.

“Hapa tulipo hatufuati utawala wa Tanzania bali tupo katika Serikali ya Magadini, kwani hakuna demokrasia hapa, neno lao ni amri, wanakamata watu, wanawafungulia mashtaka, wanawafunga au anawapiga faini,” anasema mkazi mwingine wa kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina la Lazaro.

Ukosefu wa chakula

Hali ya maisha Magadini si nzuri kwa sababu ya ukosefu wa chakula.  Mkuu wa Wilaya alipotangaza kufungwa Bwawa la Nyumba ya Mungu, wanakijiji walitoa kilio chao kuwa maisha kwao yatakuwa magumu kwa sababu chanzo chao cha mapato kitafungwa.  

Mkuu wa Wilaya aliwaambia kuwa atawapelekea chakula cha msaada baada ya wiki moja, ahadi hiyo hadi sasa haijatekelezwa.

“Hapa kwetu ardhi ni kavu, huwezi kulima kitu hapa, tunaishi mbugani.  Tunaishi kama ndege, tunatoka asubuhi tunakwenda kuhemea, tukipata chakula tunarudi tunduni jioni, na kwa kawaida familia nyingi hapa zinakula mlo mmoja tu,” alieleza Mzee Kishia.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho, anasema eneo lake lina kaya 826, lakini hivi sasa wakuu wengi wa kaya hizo wamelazimika kwenda maeneo mengine yenye maziwa na mabwawa kutafuta maisha.

“Familia nyingi hapa sasa zimebaki na watoto tu, baba zao wameondoka hapa kijijini kwenda katika maeneo mengine kutafuta riziki, wakipata fedha kidogo huwatumia watoto wao kwa njia ya Tigopesa au M-pesa,” anasema Tengelemingi.

Naye Mzee Paulo Kipaini anasema kipato cha wananchi wanaoishi kandokando ya Bwawa la Nyumba ya Mungu kimeshuka, hivi sasa wengi wanashindwa hata kulipa ada ya shule ya watoto wao.

“Watoto wetu wamerudishwa nyumbani kutokana na kukosa ada, kwa kawaida tunatakiwa kupeleka shule debe sita za mahindi, debe tatu za maharage na Sh60,000 kwa mwaka, lakini sasa hivi hatuna fedha za kununulia chakula wala hatuna fedha za michango ya shule,” anasema Kipaini.  

Mwadawa Mdee, Mkazi wa Korongo, kijijini Magadini, katika Wilaya ya Simanjiro, anasema maisha kitongojini hapo sasa hivi ni magumu kwa sababu kazi kubwa ya wakazi wa hapo ni uvuvi, lakini sasa Serikali imewakataza kuvua kwa sababu ya uvuvi haramu unaoendelea.

Mwadawa anasema Serikali imefanya vyema kuzuia shughuli za uvuvi katika Bwawa la Nyumba ya Mungu kwa sababu uvuvi unaofanywa, unahatarisha mazingira, lakini hata hivyo, wakazi wa vitongoji vilivyo pembezoni mwa Bwawa la hilo, wameathirika kiuchumi.

“Hali ni ngumu, wanaume wanalazimika kuacha familia zao kwenda maeneo mengine kutafuta maisha.  Kusema kweli maisha yetu yamekuwa ya kubangaiza, ukipata mlo mmoja unashukuru,” Mwadawa anaeleza.

Kauli ya Serikali

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Khalid Mandya,  anasema kuwa ni kweli alifika Magadini Februari 13 mwaka huu na kutoa amri ya kulifunga bwawa hilo na kuahidi kuwapelekea wananchi chakula cha msaada, lakini chakula hicho si kwa sababu ya kufungwa kwa bwawa, bali ni kutokana na ukame uliosababisha uhaba wa chakula ndani ya wilaya tatu ambazo ni Simanjiro, Mwanga na Moshi.

“Kweli tuliahidi kupeleka chakula, lakini si kwasababu ya kufungwa kwa Bwawa la Nyumba ya Mungu,  bali ni kwa sababu ya uhaba wa chakula uliokabili maeneo hayo.  Chakula cha msaada bado hatujakipeleka kwa sababu bado hakijapatikana, kikipatikana tu tutakipeleka,” anasema Mandya.

Kuhusu tatizo la uvuvi haramu katika Bwawa la Nyumba ya Mungu, Mandya anasema wanajipanga kama mkoa wa Kilimanjaro na Manyara kulishughulikia tatizo hilo.

“Tulilifunga bwawa si kwa sababu hatutaki wananchi wavue, bali kwa sababu hakuna cha kuvua, samaki wamekwisha na hata maji ya bwawa yamepungua kutokana na uharibifu wa mazingira, hivyo tunajipanga kukabiliana na tatizo hili la uharibifu wa mazingira kikamilifu kama mikoa.
“Karibuni tutaanzisha doria kali kuzungukia vijiji na vitongoji vyote vilivyo kandokando ya bwawa ili kudhibiti uvuvi haramu,” alieleza Mandya.

Tatizo la maji

Mzee Jeremiah Tengelemingi, anasema Korongo imetengwa, haina maendeleo, mbali na shida hiyo ya chakula hata maji ni shida, hivi sasa wananunua dumu moja la maji kwa Sh700 maji ambayo hutolewa Moshi na kuletwa kijijini kwao kwa baiskeli au pikipiki.

“Maji ya bwawa hatuwezi kuyanywa kwa sababu si salama.  Takataka zote za viwandani zinaingia bwawani na mvua ikinyesha inasomba uchafu wote wa milimani na kutumbukiza bwawani, hivyo hatuwezi kuyanywa maji haya,” anasema Tengelemingi.

Sehemu kubwa ya Bwawa la Nyumba ya Mungu imekauka na hata mvua zilizotarajiwa kunyesha kuanzia katikati ya Machi, hazijanyesha mpaka sasa, hivyo ukame unatishia amani mkoani Kilimanjaro kwani hata wafugaji wanalazimika kupeleka mifugo yao mbali kutafuta malisho.

Hata hivyo si kama Serikali haitambui tatizo la maji katika kijiji cha Magadini na vijiji vinginevyo, kwani Serikali ilishatoa tenda ya kutandaza mabomba kuyafikisha katika vitongoji vyote vya Magadini ili viweze kupata maji, lakini tuhuma zilizopo ni kuwa wajanja wameuhujumu mradi huo kwani wametandaza mabomba mabovu yaliyopasuka.

“Mabomba yametandazwa lakini hayatoi maji kwa sababu ni mabovu, hii ni hujuma ya makusudi na inaonyesha kuwa wako waliofaidika na mradi huu,” alisema Fraiko Kihedu, Katibu wa Kamati ya Kitongoji cha Korongo.

Kihedu, anasema tatizo la Magadini ni kwamba wananchi hawana pahali pa kukimbilia kwenda kueleza kero zao, na mara nyingi uongozi wa kijiji umekuwa ukiwatishia uhai wananchi.

“Uongozi hautaki kukosolewa wala kushauriwa, wanafanya wanavyotaka na wanaamua yale yenye maslahi kwao tu na wala si maslahi kwa wanakijiji,” alidai Kihedu.

Ahadi isiyotekelezeka
Baada ya kuona kuwa madhila yamezidi hasa kwa wakazi wa kitongoji cha Korongo,  wameandika barua kwa kijiji hadi wilayani kuomba Korongo ipewe hadhi ya kijiji kwa sababu inatimiza masharti yote ya kuwa kijiji.

“Hapa Korongo tuna kaya 862, wakati eneo linaweza kuwa kijiji kwa kuwa na kaya 250 tu, ombi hilo limekuwapo kwa zaidi ya miaka 15 sasa lakini halitiliwi maanani,” alisema Kihedu.

Aidha Kihedu anasema wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, waliokuwa wakiomba uongozi waliwaahidi wakazi wa Korongo kuwa wakiingia madarakani watahakikisha kuwa Korongo inapewa hadhi ya kijiji, lakini hadi sasa hakuna hata dalili ya wakazi wa Korongo kutekelezewa dai lao hilo.

“Huku Magadini shughuli zinazoingiza kipato ni mchanga na samaki.  Huku kuna machimbo ya mchanga, lakini cha ajabu ni kuwa kipato kitokanacho na mchanga, hakiwanufaishi wananchi.

Mchanga umekuwa ni mradi wa wakubwa, kipato chake hakiakisi katika maendeleo ya kijiji chetu,”  Kihedu alieleza
Ewura yaingilia mgogoro wa mafuta

 Fidelis Butahe  MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imeingilia kati mgogoro ulioibuka katika Kamati ya Kuratibu Uagizaji Mafuta (PIC) kutokana na wajumbe wa kamati hiyo kutoelewana.  Kutokana na mgogoro huo Ewura imeiandikia barua kamati hiyo ikiitaka kufanya kazi kwa pamoja ili kufanikisha mradi huo. Katika barua hiyo ya Machi 16, mwaka huu, iliyotiwa saini na Anastas Mbawala kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu inaeleza kuwa mamlaka imepokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa PIC kuhusu kutoelewana na mwenyekiti wao.   “Miongoni mwa sababu za kutoelewana ni kuhusu usalama wa nishati hiyo na bei ya kununua na kuuza” ilieleza sehemu ya barua hiyo.   Katika barua hiyo, PIC inaelekezwa kufanya ajira ya menejimenti ya kudumu na watumishi wengine.   “Ewura imeliona na kulichukulia suala la ajira ya menejimenti ya kudumu ya PIC na watumishi wengine kuwa la muhimu, lakini limechukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa.”,    “Kuendelea kucheleweshwa kwa jambo hilo kunaweza kuathiri ufanisi wa mpango mzima wa kuagiza mafuta kwa pamoja,” ilieleza taarifa hiyo.   Katika barua hiyo Ewura imeielekeza Bodi ya PIC  kuunda menejimenti ya kudumu ndani ya siku saba tangu kuandikwa kwa barua hiyo.  Moja ya mambo yalioamuliwa ili kupunguza bei ya mafuta ni pamoja na kuwa na mpango wa kuagiza mafuta kwa pamoja.  Baadhi ya wafanyabiashara hao wameipongeza serikali hasa Wizara ya Nishati na Madini kwa kuwa na mpango huo kwa kuwa utapunguza baadhi ya gharama.   Gharama zilizopungua ni muda wa meli kusubiri kushusha mafuta bandarini Dar es Salaam. Muda huo umepungua kutoka wastani wa siku 40 mwaka 2011 hadi siku nane hivi sasa.   Bei ya petroli hadi jana nchini ilikuwa Sh2,144 kwa lita na dizeli ilikuwa Sh2,093.   
 Sitta awashangaa CCM wanamhofia kwa nafasi hiyo
Fidelis Butahe 
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Zitto Kabwe ameibuka na kusema kuwa anataka kuwa rais wa Tanzania mwaka 2015.Wakati Zitto akitoa kauli hiyo nzito, Waziri  wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta naye amesema anashangazwa na watu wanaoweweseka wanaposikia kuwa mwanasiasa huyo anayeongoza vita dhidi ya ufisadi ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, anataka kuwania urais.

Kauli hiyo ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni huenda ikaibua mjadala mzito ndani ya chama chake, ukiacha zile mbio za vigogo wa CCM wanaotajwa kuutaka urais 2015. 

Katika taarifa yake aliyoituma jana kwa gazeti la Mwananchi Jumapili, Zitto alisema; “ Kwanza niseme wazi kabisa kuwa Urais ninautaka, nchi inahitaji kiongozi wa juu atakayekabili changamoto hizi. Ninaamini ninaweza kuwaongoza Watanzania wenzangu kukabili changamoto hizi.”  Alitamba anao uwezo kwa kuwa ni mzalendo, mwenye utashi wa kuleta mabadiliko stahiki kulingana na nchi inavyoongozwa.   Katika taarifa hiyo ameeleza kuwa kwa sasa nchi imesahau maendeleo ya watu badala yake imejikita katika maendeleo ya vitu.

 “Ninajua kuwa hivi sasa viongozi wetu wengi wanaangalia zaidi mitindo badala ya mambo ya msingi,” Zitto amesema taarifa na kuongeza:   “Ninajua kuwa maendeleo vijijini yamesahaulika, ninajua nchi yetu inahitaji uongozi wa kufanya mabadiliko makubwa badala ya mabadiliko ya juujuu.” 
Alieleza kuwa mabadiliko makubwa  yanahitaji  maamuzi magumu yatakayoudhi wengi hasa vigogo wa nchi za Magharibi huku akitoa mfano kuwa ni pamoja na kuzuia nchi kuuza malighafi pekee.   Alisisitiza kuwa rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma ndio kikwazo kikubwa cha maendeleo ya nchi na kwamba lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia na kutokomeza ufisadi.  

“Rasilimali kama madini, mafuta, gesi asilia, ardhi na nyinginezo ni lazima zifaidishe wananchi wa nchi yetu,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.  Sababu za kutaka  Urais  Katika taarifa hiyo Zitto alieleza kuwa kwa sasa nchi inahitaji kiongozi wa juu atakayekabili changamoto muhimu na kwamba yeye anaweza kuwaongoza Watanzania kukabiliana na changamoto hizo.  “Sio kazi rahisi, lakini ni kazi ambayo lazima Mtanzania mmoja aifanye, mimi nataka kuifanya, nina uwezo wa kuifanya,” alitamba katika taarifa hiyo.

 Alieleza kuwa hata kama anaitaka kazi hiyo, ni lazima Watanzania walio wengi  waamue, pia ni lazima Chadema kiseme wazi kuwa yeye ndio anastahili kuifanya kazi hiyo na kwamba kuitaka tu nafasi hiyo hakutoshi bila ridhaa hizo.   “Kama wananchi watasema huyu Zitto anapaswa kubeba jukumu hili mwaka 2015 tuache iwe. Kama watasema hapana wewe bado mpaka mwaka 2020 au 2025 tuache iwe hivyo. Pia Kama hawataki kabisa tuache iwe hivyo,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

   Umri wa kugombea urais  Katika taarifa hiyo, Zitto alieleza kuwa mjadala wa umri wa kugombea urais umekuwa mkali na kwamba baadhi ya watu kwa sababu zao binafsi, wameamua kuuita ni mjadala wake na Mbunge wa Bumbuli January Makamba ambao unaowabagua wazee.  
Alisema kuwa mjadala huo aliouita wa ‘kupandikiza chuki na sumu za kibaguzi’ ni wa kitabaka, unaonyesha kuwa Zitto na January sio tabaka stahili la vijana walio wengi.  Huku akionyesha kujibu makala katika moja ya magazeti(sio ya Mwananchi Communications Limited) ambayo haikupinga umri bali hoja ya wanaoujadili urais na vyama wanavyotoka kutowapika vilivyo vijana kuwa viongozi, Zitto alieleza kuwa hali hiyo inaonyesha ubaguzi wa wazi.

   “Ingawa sisi sio waanzilishi wa hoja hii lakini ni hoja ya kibaguzi. Nawashangaa wasomi wa siku hizi kwa kujadili watu badala ya hoja,” ilieleza taarifa hiyo.  Chadema kukuza vijana  Alieleza kuwa Chadema kinalea na kukuza vijana kuwa viongozi na kwamba yeye alijiunga na chama hicho akiwa na umri wa miaka 16 huku akipewa majukumu mbalimbali. 
Alisema kuwa wakati akisoma Chuo Kikuu Dar es Salaam(UDSM), Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wakati huo akiwa Mbunge wa Jimbo la Hai, alimuomba kushiriki kikamilifu kukijenga chama hicho kutokana na kukimbiwa na wanachama isipokuwa wale waliokuwa wakitokea Kigoma, Kilimanjaro, Shinyanga, Karatu na Ukerewe.  

“Mwaka 2001 muongo mmoja uliopita ni mimi na Mbowe ndio tuliofanya mabadiliko yote yanayoonekana Chadema.  Tumeingiza watu wapya na tumeandika Katiba upya, tulichambua mambo mengi na Mbowe kuijenga Chadema,” alieleza katika  taarifa hiyo.  

Alieleza kuwa mwaka 2005 Mbowe aligombea urais na kwamba walijua kuwa watashindwa ila walitaka kukijenga chama hicho na walipata wabunge na kuongeza kuwa mwaka 2010, Chadema kilishiriki  uchaguzi mkuu kama chama imara kinachokwenda kuchukua dola.  Huo ndio ukawa mwanzo wa kuibuka kwa wabunge John Mnyika (Ubungo), Halima Mdee (Kawe), wabunge ambao alieleza kuwa awali walionyesha wasiwasi mkubwa kujiingiza katika siasa. 
“Baadhi ya watu wazima waliingia Chadema kwa sababu ya vijana, nani anasema hatulei vijana kuwa viongozi wazuri, nani haoni hazina ya viongozi vijana hivi sasa ndani ya Bunge kutoka vyama vyote. Kuna namna bora ya kulea viongozi zaidi ya kuwapa majukumu?” Alihoji katika taarifa hiyo.

Hoja ijadiliwe  Katika taarifa hiyo Zitto alifafanua kuwa hoja ya umri wa kugombea urais iwe na mahali pakuanzia na inapaswa kujadiliwa bila kuangalia majina ya wanaotetea hoja hiyo.   Suala hilo lijadiliwe kwa faida na hasara zake na kufafanua kuwa hakuna anayejua kuwa yeye atakuwa hai mwaka 2015 na kwamba isiandikwe katiba  yenye kupanua wigo wa kutoa haki ya kugombea urais kwa sababu yake.
Samuel Sitta

Akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali katika Tamasha Vyombo vya Habari lililofanyika jana kwenye Ukumbi Msasanki Beach, Dar es Salaam, Sitta alieleza kuwa anashangazwa na watu wanaoweweseka wakisikia anataka kuwania urais mwaka 2015.

"Nashangaa watu wanapata kiwewe kusikia nataka kuwania urais, kuwania urais ni haki ya kila Mtanzania na Watanzania ndiyo watakaoamua nani ni mzuri na atawafaa," alisema Sitta na kushangiliwa na waliohudhuria tamasha hilo.

"2015 tunataka kuwa na mwelekeo mzuri, nikiwa na maana mambo ya hongo, ubadhirifu hatutaki yawe na nafasi, alisema Sitta na kuongeza:

"Kuna hadithi moja, siku moja trafiki mmoja alikamata gari pale Mwenge (Dar es Salaam) akaomba, leseni, akaangalia kadi ya gari sasa yule mama alikuwa na mtoto wake ana miaka kama minane, akamwambia mama yake, mpe kitu kidogo...hivi imefikia hatua hata mtoto wa miaka minane anajua rushwa."

Alisema rushwa imesababisha nchi kuingia mikataba ya uongo, kuna mikataba mingi ya uongo na ndio maana  leo hii nchi imefika hapa ilipo.

"Hii imesababisha matatizo hadi ya umeme, tungeweza kuuza umeme wetu nje, lakini leo haiwezekani, nasema haya kama mzee wenu na kiongozi wenu.

"Sasa, nawaasa waandishi, msikubali kuwa mawakala wa viongozi waongo, msikubali uongo na kama tungeendelea kule uongo, nchi ingeharibika...hatuwezi kusonga mbele kwa uongo na vyombo vyenu visitumike kusambaza mambo ya uongo," Sitta alishauri.
 ADAIWA KUPIGWA 'STOP' ASISHIRIKI,ASEMA NI UZUSHI WA KIPUUZI, CHADEMA WALIAWaandishi Wetu, Arumeru na Dar USHIRIKI wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge Arumeru Mashariki unadaiwa kuigawa timu ya kampeni ya CCM inayomnadi mgombea wa chama hicho, Sioi Sumari.Lowassa ambaye yuko mkoani Arusha tangu Machi 20, mwaka huu, amekuwa akitajwa kwamba atamnadi Sioi lakini tofauti na makada wengine, hadi sasa hakuna ratiba yoyote ndani ya CCM inayoonyesha ni lini mbunge huyo wa Monduli atapanda jukwaani.Habari zilizopatikana jana kutoka Arumeru na Dar es Salaam zinasema baadhi ya viongozi wa CCM na timu inayoongoza kampeni za uchaguzi huo wamegawanyika kuhusu Lowassa kupanda jukwaani, huku wengine wakipinga.Kumekuwepo na kundi ambalo linaona kwamba Lowassa akiingia kwenye kampeni hizo anaweza kuzua mazingira  ambayo yataipa ugumu CCM kushinda kutokana na kumbukumbu kuwa alijiuzulu kutokana na kashfa ya utoaji wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura iliyotolewa kwa kampuni tata ya Richmond Development LCC.Chadema tayari kimetangaza kuwa endapo Lowassa atajitokeza kwenye kampeni hizo kumnadi mgombea wa CCM, watamuumbua kwa kile wanachodai wataweka hadharani tuhuma kinazodai zinamhusu.Jana, mmoja wa viongozi wa chama hicho alisema: “Hatapanda jukwaani (Lowassa), wala hatothubutu kufanya hivyo kwani tayari ameambiwa aache na huyo aliyemwambia nadhani anamsikiliza, hawezi kukiuka.” Kauli ya kiongozi huyo inafanana na ile iliyotolewa na mmoja wa makada wakongwe wa CCM anayeshiriki kampeni za Arumeru Mashariki ambaye Machi 20 mwaka huu akiwa Usa River alsikika akisema: "Lowassa hana umuhimu wowote” kwenye kampeni hizo. Kiongozi huyo alikuwa akichangia mjadala usio rasmi uliokuwa ukiwahusisha makada kadhaa wakongwe wa CCM, walipokuwa wakisubiri kuanza kwa msafara wa kwenda kwenye moja ya mikutano ya kampeni.Lowassa ajibuAkizungumza kwa simu kuhusu madai hayo jana, Lowassa aliziita taarifa za kukatazwa kwake kupanda jukwaani kumnadi Sioi kuwa ni “uzushi usiokuwa na msingi.” Hata hivyo, hakuwa tayari kuweka bayana aina ya ushiriki wake kwenye kampeni hizo zinazoelekea ukingoni, huku CCM kikikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mahasimu wao Chadema ambacho kimemsimamisha, Joshua Nassari.“Kwani kuna nini, hakuna haja ya kuwa na haraka, kwani vyovyote itakavyokuwa mtajua tu,” alisema Lowassa.Mapema jana asubuhi alipotafutwa kwa simu, Lowassa alisema asingeweza kuzungumza kwani alikuwa kwenye kikao. “Nipigie majira ya mchana kama saa tisa hivi, maana sasa niko kwenye kikao,” alisema.Hata hivyo, watu walio karibu na kiongozi huyo walisema Lowassa atapanda jukwaani kesho na kwamba tayari ameanza kampeni za kumnadi Sioi kwa kufanya vikao vya ndani na kwamba kikao cha jana ni moja ya vikao hivyo.“Hizo taarifa kwamba amezuiwa siyo za kweli, mimi nimehakikishiwa kwamba atapanda jukwaani kuanzia Jumapili (kesho) na ninavyofahamu tayari ameanza vikao vya ndani,” alisema mmoja wa watu wa karibu na Lowassa.Mwana CCM mwingine aliye karibu na kiongozi huyo alisema: “Ni kweli walikuwa wakihaha kumzuia, eti wandai kwamba ushindi ukipatikana itaonekana kwamba ni mafanikio yake, lakini wameshindwa maana hadi sasa tuna uhakika Mzee (Lowassa) atapanda jukwaani."Habari zaidi zinasema kuwa Mratibu wa Kampenzi za CCM katika uchaguzi huo, Mwigulu Nchemba juzi jioni alikutana na Lowassa kuweka mambo sawa kabla ya kiongozi huyo kupanda jukwaani kesho.Timu ya kampeniTangu kuanza kwa kampeni hizo,inadaiwa kwamba kumekuwapo na hali ya kutokuaminiana ndani ya timu hiyo kunakotokana na kile kilichojiri wakati wa mchakato wa kura za maoni zilizompa ushindi Sioi.“Tatizo kubwa hapa kwetu ni hilo, hawa wapambe wa mgombea hawaamini kwamba sisi wengine tumekuja kwa ajili ya kutafuta ushindi wa chama, wanatufikiria vinginevyo ndiyo maana unaweza kuona kama tuko makundi tofauti,” alisema mmoja wa makada waliopo Arumeru ambao wanashiriki kampeni hizo.Kada huyo alisema awali ni kama kulikuwa na timu mbili za kampeni ambazo ni ile ya chama inayoongozwa na Nchemba na timu ya pili ni ile inayoongozwa na wapambe wa mgombea ambao walikuwa na wasiwasi kwamba mgombea wao anaweza kuhujumiwa.“Lakini sasa naona kama imani inarejea taratibu, wanatuona tunavyochapa kazi na kumpigia kampeni mgombea wetu. Wasichofahamu ni kwamba msuguano huwa kwenye vikao tu, lakini mtu akishateuliwa hakuna haja ya kumpinga kwani kufanya hivyo ni kukiua chama chetu,” alisema kada huyo.Hata hivyo, kada huyo alisema pamoja na misukosuko ya hapa na pale, kampeni zao zimekuwa zikiimarika kila kukicha na kwamba wana uhakika wa kushinda kiti hicho cha ubunge ambacho kiko wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wake, Jeremia Sumari.Chadema waliaKatibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa jana alilalamikia kile alichodai kuwa ni kuchezewa mchezo mchafu na makada wa CCM. Malalamiko ya Dk Slaa yanatokana na  kusambazwa barua yenye nembo ya Chadema ambayo ina maneno ya kashfa dhidi ya Meneja Mwenza wa kampeni wa chama hicho, Vincent Nyerere.Akizungumza kwenye mikutano ya hadhara katika Vijiji vya Nkoanekoli, Kata ya Nkoaranga, Kikwe na Akheri, Dk Slaa alisema amesikitishwa na barua hiyo iliyosambazwa usiku wa manane maeneo ya Tengeru na Leganga.“Barua hii inaonyesha kama imeandikwa na Naibu Katibu Mkuu wa  Chadema, Zitto Kabwe lakini cha ajabu jina langu limekosewa limeandikwa Silaha wakati siitwi hivyo na imeghushiwa nembo na kumbukumbu ya chama changu. Huu ni wizi ambao haukubaliki hata kisheria,” alisema Dk Slaa.Akinukuu barua hiyo, Dk Slaa alisema maneno yake yanamshauri kuachana na Vicent Nyerere kwa sababu amemchafua Mkapa, anayeheshimika Meru na nchi nzima, hivyo hali hiyo itasababisha kukosa kura Meru.“Sisi tumechukua barua hizi na nakala tumepeleka polisi na namtaka Isaya Mngulu amtafute mhusika wa barua hii ili ashughulikiwe kwa sababu kughushi nembo ni kosa kisheria na njia za kumpata ni rahisi sababu anatafutwa hata kwa njia ya kompyuta,” alisema.Dk Slaa alisema kuwa ugomvi wake siyo kukosewa jina lake wala kumchafua Nyerere, sababu watake wasitake Nyerere ni mtoto wa baba mkubwa wa marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, hivyo hakuna uhusiano na uchaguzi huo.Alisema ugomvi wake ni kughushi nembo hiyo ya chama na amegundua imeghushiwa baada ya kuwasiliana na Zitto ambaye alikana kuandika barua hiyo wala kuifahamu. Zitto akizungumza kwenye mkutano wa hadhara jana pia alikana kuitambua barua hiyo.
 Lundenga: Ni mwanzo wa mafanikio ya Redds Miss tz 2012 Imani MakongoroHUENDA mfumo huu ukawa mgeni lakini ukweli ni kwamba, Miss World kuanzia mwaka huu na kuendelea itakuwa ikifanyika Agosti na washiriki watatakiwa kuripoti kambini mwezi mmoja kabla yaani Julai.Utaratibu huu umetokana na mabadiliko ya kalenda ya waandaaji wa mashindano hayo, ambapo miaka iliyopita shindano hilo lilikuwa likifanyika Desemba na washiriki kutakiwa kuripoti Novemba.Kulingana na mabadiliko hayo Tanzania itatuma mwakilishi kwenye mashindano ya dunia ya mwaka huu, atapatikana kwa kuwapambanisha warembo 10 jukwaani wakati huo huo mchakato wa kumpata Redds Miss Tanzania 2012 utakuwa ukiendelea kama kawaida.    Miss Tanzania mbili ndani ya mwaka mmoja:Hashim 'Uncle' Lendenga  anasema kwamba, wameamua kufanya hivyo ili Tanzania iweze kuwa na mwakilishi kwenye Miss World  ya 2012."Miss Tanzania hufanyika  Septemba miaka yote, mabadiliko ya kalenda ya Miss World yanaonyesha shindano litakuwa likifanyika Agosti kila mwaka na washiriki kutakiwa kuwasili China (yanapofanyika mashindano) Julai," alisema.    Nani atapeperusha bendera ya Tanzania kwenye Miss World 2012."Tutafanya shindano dogo litakalohusisha warembo 10 kwenye fainali na mshindi ndiye atakuwa mwakilishi wetu kwenye Miss World," anasema Lundenga.Anasema mchakato wa kumpata mlimbwende huyu utakuwa wa usaili ambapo watawafanyia usaili warembo kati ya 40 hadi 50 ili kupata 10 bora watakaowekwa kambi ya siku chache kabla ya fainali itakayofanyika Mei.     Mchakato halali wa Miss Tz utakuwaje."Wakati hayo yakiendelea pia mchakato uliozoeleka wa kumpata Redds Miss Tz 2012 utakuwa ukiendelea," anasema.Anasema zoezi hilo halitakuwa na tofauti na Miss Tz zilizopita ambapo mchakato utaanzia ngazi za vitongoji, kanda na hatimaye taifa katika fainali itakayowakutanisha warembo kati ya 28 na 29."Fainali itafanyika Septemba kama ilivyoada lakini mshindi atakayepatikana atapeperusha bendera ya Tanzania kwenye Miss World ya 2013 itakayofanyika Agosti," anasema.    Mabadiliko ya Miss World yameiathiri vipi tz."Kwanza yamevuruga ule utaratibu wa kumpata mwakilishi wetu kwenye Miss World ingawa Kamati iliamua kutumia utaratibu wa kutuma mwakilishi hivyo haijatuathiri sana," anasema.Anasema pamoja na hilo mabadiliko hayo yamevunja utaratibu wa mshiriki kupewa mwaka mmoja kwa kutoa'second chance' kwa warembo waliopita ambao wanavigezo kujaribu tena bahati yao na wale ambao bado lakini wana vigezo kuitumia nafasi hiyo."Mwakilishi wetu mwaka huu atakuwa na muda mfupi mno wa maandalizi kabla ya kuondoka kwenda kwenye fainali sambamba na kuwa kambini kwa siku chache tofauti na ilivyozoeleka," anasema.        Tanzania itanufaika vipi na mabadiliko hayo kwenye Miss World ya 2013.  Lundenga anasema pamoja na mabadiliko hayo kuiathiri Tanzania mwaka huu lakini pia  yatakuwa na manufaa kwa Redds Miss Tanzania 2012 kwenye Miss World ya 2013."Kwanza kabisa mrembo wetu atakuwa na muda mwingi wa kufanya maandalizi yake kabla ya kushiriki Miss World," anasema.Anasema pia mrembo huyo atakuwa na nafasi ya kufanya kazi za kijamii pamoja na kujifunza mbinu mbalimbali za kimataifa ambazo zitamuweka kwenye nafasi nzuri katika Miss World ya 2013."Mabadiliko hayo si kwa Redds Miss Tanzania 2012 hata kwa warembo wengine watakaofuata watakuwa na nafasi ya kufanya vizuri kwa kuwa watakuwa na muda mrefu wa maandalizi yao," anasema.Kwa mara ya kwanza Tanzania ilifanya vizuri kwenye Miss World ya 2005 kwa Nancy Sumari kuingia hatua ya tano bora akiwa miongoni mwa washiriki kutoka nchi 120 na kuiwezesha nchi kupanda kwenye chati ya viwango vya ubora vya urembo vya dunia.